Friday, May 30, 2014

Kuanzia Sasa Vigodoro Vimepigwa Marufuku Dar es Salaam


Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam limepiga marufuku ngoma za kitamaduni ambazo zimekuwa zikifanyika  nyakati za usiku kwenye maeneo mbalimbali Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa kukabiliana makundi ya kihalifu ambayo yamekua tishio kwa usalama wa raia.
Kufuatia kuibuka kwa makundi ya kihalifu kama Panya road na Mbwa mwitu ambayo wengi wao wanahusishwa na ngoma hiyo kwenye uporaji na upigaji wa watu, Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova anasema ‘ni marufuku kwa ngoma yeyote ya asili kuchezwa nyakati za usiku’

Kamanda Kova anasema kufuatia operesheni inayoendeshwa dhidi ya vikundi hivyo vya kihalifu, mpaka sasa tayari wanawashikilia wafuasi zaidi ya mia moja ambapo pia watu wengi wamekuwa wakilalamikia vitendo viovu vinavyofanyika nyakati za usiku wakati wa ngoma hizo maarufu kama ‘vigodoro’ pamoja ‘baikoko’ na sasa jeshi la polisi limetoa onyo kali kwa watakaoendeleza hizi ngoma kuanzia sasa.


Mrembo Anaswa akiwa amevaa Nguo za Kuambiana

Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
AMA kweli duniani kuna sarakasi! Takribani siku kumi tangu alipofariki dunia aliyekuwa ‘kichwa’ kwenye filamu za Kibongo, Adam Phillip Kuambiana (38), mrembo aliyejitambulisha kwa jina Mary Njombe amenaswa na nguo za staa huyo wakati mali za marehemu hazijagawanywa.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu makini, Mary ambaye ni mkazi wa Magomeni Hospitali, Dar amekuwa akipigilia pamba za marehemu hasa baada ya jamaa huyo kutangulia mbele ya haki.
“Jamani njooni huku Magomeni Hospitali hapa mtaa wa pili kuna mwanamke anatinga nguo za marehemu Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu walifanya msako eneo hilo hadi wakamnasa Mary.
Katika mahojiano na gazeti hili, Mary alisema kuwa alikuwa mchumba wa Kuambiana na alichobahatika kubaki nacho ni nguo ambazo alimpatia mara ya mwisho amfulie (zinaonekana pichani).

Mary alisema kuwa yeye na Kuambiana walifahamiana tangu mwaka 2006 ambapo alikuwa akimbembeleza kuwa naye.

“Mwaka 2008 ndiyo tulianza rasmi uhusiano kwani mimi nilikuwa sina mwanaume na yeye hakuwa na mtu hivyo tulikubaliana na alikuwa akijulikana nyumbani kwetu,” alifunguka Mary.

Mwanadada huyo alisema kuwa yeye na Kuambiana walikuwa wakikutana kwenye Hoteli ya Grand iliyopo Magomeni, Dar na mara nyingi alikuwa akimpikia chakula na kumpelekea ‘lokesheni’.
“Nimeumia sana na sijielewi, Kuambiana ameniachia donda kubwa, nakumbuka neno la mwisho aliniambia nimpende sana kwani ipo siku nitamkubuka,” alisema Mary huku akiangua kilio.

Alipoulizwa kama kweli nguo hizo ni za marehemu Kuambiana, alizama ndani akatoka akiwa amevaa pensi na shati la ‘drafti’ alilokuwa anapendelea kulivaa staa huyo ambalo ni maarufu sana.
Kuambiana alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 17, mwaka huu baada ya kuanguka chooni kutokana na kusumbuliwa vidonda vya tumbo.


Thursday, May 1, 2014

Baadhi ya Magazeti ya leo Tar 1 May, 2015

HII NDIO NCHI ILIYOPITISHA SHERIA YA WEZI KUKATWA MIKONO NA WAZINIFU KUPIGWA MAWE

Sultani na mtawala wa Brunei ambaye ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani


Serikali ya Brunei iliyo Kusini Mashariki mwa Bara Asia, itaanza kutumia sheria kali za kiisilamu.

Kiongozi wa nchi hiyo ya kiisilamu ambayo ni jirani na Malaysia ametangaza kuwa sheria hiyo itaanza kutumika kuanzia wiki hii.

Adhabu zilizo chini ya sheria za kiisilamu ni pamoja na kuwakata wezi mikono na kuwapiga mawe hadi kufa watu waliopatikana na hatia ya kushiriki Zinaa.
Sheria hii itatekelzwa katika awamu tatu katika kipindi cha miaka mitatu.
Umoja wa Mataifa tayari umeelezea wasiwasi wake kuhusu sheria hiyo.
Taifa la Brunei tayari linafuata sheria kali za kiisilamu kuliko hata nchi jirani kama Malaysia na Indonesia pamoja na kuharamisha uuzaji na utumiaji wa pombe.
Nchi hiyo ndogo ilio katika kisiwa cha Borneo,inatawaliwa na Sultan Hassanal Bolkiah na imepata utajiri wake kutokana na kuuza nje mafuta na gesi yake.
Takriban nusu ya waisilamu wanaoishi katika nchi hiyo ni raia wa Malaysia.
Sultani alinukuliwa akitangaza hatua ya kwanza ya kuanza kutumiwa kwa sheria hiyo akimshukuru Mungu na kuwatahadharisha wananchi kuhusu kuanza kutumika kwa sheria hiyo.

Sheria yenyewe itaanza kutumika katika kipindi cha miaka mitatu huku hukumu ya makosa ya kwanza ikiwa kifungo cha jela pamoja na kutozwa faini.
Katika awamu ya pili ndipo wahalifu wataanza kukatwa mikono kwa watakaopatikana na hatia ya wizi , huku awamu ya tatu ikihusu kupigwa mawe wazinifu na wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Sultani anayetawala kisiwa hicho ni mmoja wa matajiri wakubwa duniani na tayari amewaonya watu kukoma kushambulia mipango yake kupitia mitandao ya kijamii.

Mfumo wa sheria katika mahakama nchini humo ni sawa na ule wa Uingereza.
Umoja wa Mataifa uliitaka serikali kuchelewesha mageuzi hayo ili kuhakikisha kuwa sheria hiyo inaambatana na sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu. Credits: BBC


Victoria Kimani abaki ‘topless’ kisiwani Mbudya - Picha

Victoria Kimani kiyapa utamu maji ya bahari ya Hindi kisiwani Mbudya, Dar es Salaam kwa kuyaoga bila kuvaa kitu chochote cha kusitiri  maziwa yake na kwakuwa Mungu kamjalia ‘boobs’ za kuvutia kama za Katy Perry, ilikuwa burudani tu kwa waliomshuhudia.